Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 03Article 540892

Habari za Mikoani of Thursday, 3 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Waitara asimamisha kazi vigogo wawili uzembe Mv Mbeya II

Waitara asimamisha kazi vigogo wawili uzembe Mv Mbeya II Waitara asimamisha kazi vigogo wawili uzembe Mv Mbeya II

Waitara amechukua uamuzi huo kwa madai ya kuwepo kwa uzembe uzembe wa kutotoa taarifa za tatizo kuhusu ubovu wa meli ya Mv Mbeya II tangu iliporipotiwa mapema mwaka 2020 na kiongozi wa meli hiyo na mabaharia.

Amewataja waliosimamishwa kuwa ni Kapteni wa meli kutoka makao makuu TPA, Abdalla Mwengamno na Kaimu Meneja wa Bandari Ziwa Nyasa, Hamis Nyembo.

"Mlikuwa mnatambua changamoto ya meli hii tangu mwaka jana lakini hamkutoa taarifa jambo ambalo limehatarisha usalama wa wasafiri wanaotumia meli hiyo," amesema Naibu Waziri huyo.

Amemuagiza Katibu Mkuu kukaa na bodi ya TPA kuwaondoa watumishi hao katika nafasi hizo na wawekwe wengine watakaokuwa wazalendo na kusimamia meli kwa maslahi mapana ya Taifa.

https://bit.ly/3pgkLZu

Mkurugenzi wa kampuni ya Songore Marine iliyojenga meli hiyo, Salehe Songoro, amesema kwa sasa kuna changamoto ya kifaa cha kuendeshea meli akibainisha kuwa ndani ya wiki mbili kitakuwa kimerekebishwa licha ya kuwepo matatizo mengine.

Aprili 3, 2021 meli hiyo ikiwa safarini ilipigwa na mawimbi na kukwama kwenye mchanga huku Mkuu wa Wilaya ya Kyela mkoani humo, Claudia Kitta, akisema ilikuwa na abiria 87 na wote walitoka samala.

https://bit.ly/2S5IEqA

Join our Newsletter