Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 22Article 573562

Habari Kuu of Monday, 22 November 2021

Chanzo: ippmedia.com

Wajumbe wa Bodi CRB watembelea mradi wa Megawati 2,115

Wajumbe wa Bodi CRB watembelea mradi wa Megawati 2,115 Wajumbe wa Bodi CRB watembelea mradi wa Megawati 2,115

Wajumbe wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), imetembelea mradi wa mkubwa wa bwawa la kufua umeme wa maji la Julius Nyerere (JNHPP) uliiopo Rufiji mkoani Pwani.

Kampuni hizo mbili za kigeni zinatekeleza mradi huo chini ya usimamizi wa Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme (TANESCO) na  Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS).

Wajumbe hao wa Bodi wakiongozwa na Mwenyekiti, Mhandisi Consolata Ngimbwa walionyesha kufurhishwa kwao na maendeleo ya ya mradi huo na kujifunza mambo mengi.

Pia Mwenyekiti wa Bodi ya CRB, Mhandisi Consolata Ngimbwa alizitaka kampuni hizo za kigeni kuhakikisha zinatoa nafasi za ushiriki wa miradi mbalimbali inayoitekelezwa ili kuziinua kampuni za kizalendo zilizopo nchini.

“Mradi huu ni mkubwa sana na una kazi nyingi sana hivyo anaona fursa ipo kwa makandarasi wazawa kuepwa kazi ndogo ndogo kama  sub – contractors”,” alisema.

Pia alizitaka kampuni zinazohusika na masuala ya ukandarasi hapa nchini kujenga ushirikiano wa pamoja ili kuwa na nguvu ambazo licha ya kuzisaidia kupata mitaji mikubwa itawawezesha kufanya kazi kwa kipindi kifupi na ufanisi utakaoleta matokeo chanya katika mradi husika.

 Bwawa hilo linatarajiwa kuzalisha  Megawati 2,115 na kwa sasa mradi huo umefikia asilimia 48.2 .

Kukamilika kwa mradi huo kutawezesha  Watanzania kupata umeme wa gharama nafuu ambao utasambazwa nchini kote na ziada kuuzwa nje ya nchi ili kupata faida za kigeni.