Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 19Article 552433

Habari za Mikoani of Thursday, 19 August 2021

Chanzo: MWANANCHI

Wakazi Dar kupata chanjo ya Uviko-19 Jumapili

Mkuu wa Mkoa Amos Makalla Mkuu wa Mkoa Amos Makalla

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema Jumapili Agosti 22, 2021 wakazi wa Dar es Salaam wajitokeze kupata chanjo ya Uviko-19 katika viwanja vya Uhuru kwa hiari.

Amesema mchakato utawahusu wananchi wote wenye umri wa kuanzia miaka 18 ambao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakikosa muda wa kwenda kupata huduma hiyo katika vituo vilivyoanishwa mkoani Dar es Salaam.

Makalla ameeleza hayo leo Alhamisi Agosti 19, 2021 wakati akizungumza na watendaji na wafanyakazi wa manispaa ya Temeke katika kikao kazi cha halmashauri

Katika maelezo yake, Makalla amesema kwa nyakati tofauti amekuwa akipokea ujumbe kwa njia ya mbalimbali ikiwemo kwenye mitandao ya kijamii kutoka kwa wananchi wakimueleza kukosa huduma hiyo kutokana na majukumu yaliyowakabili.

" Kilio cha chanjo hasa wanaofanya kazi kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa na kukosa muda kimesikika, sasa chanjo itatolewaa Jumapili katika eneo la wazi kuanzia saa 2 asubuhi. Tutakuwa na wahudumu 100 kwa ajili ya shughuli hii,"

" Wakuu wa Wilaya wataweka utaratibu maalumu kwa ajili ya mchakato huu. Huu ndio uongozi wa kusikiliza kilio cha wananchi, tunataka kuwasaidia watu wetu, ugonjwa upo na matukio ya watu kuugua na kufa yapo," amesema Makalla.