Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 22Article 543685

Habari za Afya of Tuesday, 22 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Wakazi Dar waitwa kupimwa macho 

Wakazi Dar waitwa kupimwa macho  Wakazi Dar waitwa kupimwa macho 

WANANCHI wa Temeke na maeneo mengine mkoani Dar es Salaam wametakiwa kujitokeza kwa kupimwa na kufanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho kwa watakaobainika ili kuondoa tatizo hilo.

Akizungumza kwa niaba ya Gondwe, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Gwamaka Mwabulambo, alisema Wilaya ya Temeke ina watu wengi wenye matatizo ya macho, hivyo akawataka kujitokeza kwa wingi kupimwa na kufanyiwa upasuaji bure kwa watakaobainika kuhitaji huduma za upasuaji.

Alisema huduma za macho zilikuwa zimesahaulika kwa muda mrefu, lakini sasa serikali inazitilia mkazo na imeipongeza jamii ya Shia kwa kusaidia kujengwa kwa kituo hicho na kutoa huduma za matibabu ya macho.

Alisema Wilaya ya Temeke yenye watu karibu milioni mbili, hicho ni kituo cha pili, kinachotoa huduma za upasuaji wa mtoto wa jicho baada ya Hospitali ya Mkoa wa Temeke, ambayo ndio pekee ilikuwa ikitoa huduma hiyo kabla ya kuzinduliwa kwa kituo hicho juzi.

Mwabulambo alisema mwaka jana watu 1,187 walifanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho wilayani humo, hivyo uzinduzi wa kituo hicho utasaidia kupunguza tatizo hilo, ambalo ni kubwa Temeke.

Naye mjumbe wa bodi iliyofanikisha ujenzi wa kituo hicho, Ain Sharrif, alisema wameamua kuweka kituo hicho Temeke kwa kuwa wilaya hiyo ndio yenye wakazi wengi, lakini aliwataka watu kutoka maeneo mengine kujitokeza kupata huduma hizo.

Sharrif alisema nia yao ni kuhakikisha tatizo la mtoto wa jicho linapungua au kumalizika kabisa wilayani Temeke na nchini kwa jumla.