Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 30Article 560497

Uhalifu & Adhabu of Thursday, 30 September 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Wakili wa serikali kuhusu kesi ya Mwakabibi

Wakili wa serikali kuhusu kesi ya Mwakabibi Wakili wa serikali kuhusu kesi ya Mwakabibi

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam Lusubilo Mwakabibi (kushoto) akiingia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza kesi inayomkabili.

KESI inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam Lusubilo Mwakabibi na mwenzake Edward Haule ambaye alikuwa mratibu wa mradi wa DMDP, imeahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hadi Oktoba 19, 2021 kutokana na upelelezi kutokamilika.Mwakabibi na mwenzake Haule wanakabiliwa na mashtaka mawili ambayo kwa mara ya kwanza walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Evodia Kyaruzi, ambapo Wakili wa Serikali Slivia Mitanto amesema kuwa upelelezi bado haujakamilika hivyo kuomba Mahakama kupanga tarehe nyingine.Katika kosa la kwanza watuhumiwa wote wawili wanashtakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi kwa kuelekeza ujenzi wa stendi ya mabasi katika kiwanja kinachomilikiwa na Kanisa la Angilikana bila ya kupewa ruhusa, kosa waliolitenda kati ya Machi 2020 na 2021.Katika kosa la pili, washtakiwa hao wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya kwa makusudi kinyume cha kifungu cha 3 kifungu kidogo cha kwanza cha Sheria ya Ardhi.