Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 31Article 554587

Habari za Mikoani of Tuesday, 31 August 2021

Chanzo: eatv.tv

Wakurugenzi wadaiwa kuficha barua za uhamisho

Wakurugenzi wadaiwa kuficha barua za uhamisho Wakurugenzi wadaiwa kuficha barua za uhamisho

Katibu Mkuu Wizara ya TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe, amekeonya tabia ya baadhi ya Wakurugenzi na watumishi wa Idara za Masijala wanaoficha barua za uhamisho ambazo tayari zimekwishasainiwa huku wakitengeneza mazingira ya viashiria vya rushwa ili waweze kukabidhi barua hizo kwa wahusika.

Profesa Shemdoe ametoa kauli hiyo mkoani Shinyanga na kusema kwamba kwa nyakati tofauti amekuwa akipokea malalamiko yasiyoisha juu ya mkwamo huo wa baadhi ya barua za uhamisho kutokuwafikia watumishi waliopata uhamisho kwa wakati.

"Kumeibuka wimbi la baadhi ya Wakurugenzi na Watumishi wa sehemu ya Masijala katika Ofisi za Mamlaka za Serikali za Mitaa kushindwa kutoa barua ambazo tayari zimesainiwa na Katibu Mkuu TAMISEMI na kutumwa kwenye Halmashauri, kwa ajili ya kuwapa wahusika lakini watu wachache kwa matakwa yao wamekuwa wakikwamisha barua kwenda kwa wahusika, hili halikubaliki na hii ni kwenda kinyume na maadili ya Utumishi wa Umma,” ameonya Profesa Shemdoe.