Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 21Article 558769

Uhalifu & Adhabu of Tuesday, 21 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Wakuu wa Majeshi Afrika Mashariki wakutana kujadili matukio ya ugaidi

Wakuu wa Majeshi Afrika Mashariki wakutana kujadili Matukio ya ugaidi Wakuu wa Majeshi Afrika Mashariki wakutana kujadili Matukio ya ugaidi

Viongozi wa ngazi za upelelezi za kijeshi kutoka Nchi Wanachama wa Jumuhiya ya Afrika Mashariki, wapo nchini Rwanda kwenye kikao cha siku mbili kujadili vitendo vya ugaidi vinavyo endelea kushuhudiwa kwenye baadhi ya nchi zinazounda jumuiya hiyo.

Hatua hii inakuja ikiwa ni baada ya kuripotiwa matukio kadhaa ya ugaidi kwa nchi wanachama, ikiwa ni pamoja na kesi za ugaidi ambazo zimefunguliwa Mahakamani.

Hata hivyo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro tarehe 08 Septemba, alikutana Mkuu wa Jeshi la Rwanda Emmanuel K. Gasana, na kujadili kuhusu namna ya kukabiliana na matukio ya uhalifu hususiani ni Ugaidi.

Hatua hii ya majeshi ya nchi wanachama kukutana inatoa taswira mpya katika kupambana na matukio ya uhalifu, huku maswali yakibaki juu ya utatuzi wa kesi za ugaidi zinazohusishwa kuwa za kisiasa, je kikao hiki kitakuja na mwarobaini wa tuhuma za kisiasa kuhusishwa na matukio ya ugaidi?