Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 22Article 543694

Habari za Afya of Tuesday, 22 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Walemavu waunganishwa katika huduma za afya 

Walemavu waunganishwa katika huduma za afya  Walemavu waunganishwa katika huduma za afya 

SERIKALI imeweka utaratibu wa kuwatambua watu wenye wlemavu (WWU) kupitia kamati za watu wenye ulemavu kuanzia ngazi ya kijiji ili kuwaunganisha katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa kadiri ya mahitaji yao.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Godwin Mollel, alibainisha hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Stella Ikupa (CCM) aliyetaka kujua serikali itaandaa lini utaratibu mzuri wa matibabu kwa watu wenye ulemavu wakati ikisubiri bima ya afya kwa wote.

Dk Mollel alisema kupitia mipango kabambe ya afya ya halmashauri, serikali imeendelea pia kuwatengea rasilimali kulingana na mahitaji yao.

Alitoa mfano wa wenye ulemavu wa ngozi ambao wanawezeshwa mafuta ya kuzuia jua ambayo kwa sasa hutengenezwa katika Hospitali ya Kanda ya KCMC na bidhaa hizi zimeingizwa katika orodha ya bidhaa za afya zinazosambazwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD).

Alisema serikali imetoa miongozo ya miundombinu ya kutolea huduma kwa kuzingatia haki za watu wenye ulemavu.

“Wizara imeendelea kutengeneza miongozo na mafunzo kwa watoa huduma ili kuwezesha na kuboresha utoaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu,” alisema.