Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 18Article 558208

Uhalifu & Adhabu of Saturday, 18 September 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Walimu Watano Mbaroni kwa Kuvujisha Mitihani

Walimu Watano Mbaroni kwa Kuvujisha Mitihani Walimu Watano Mbaroni kwa Kuvujisha Mitihani

WATU sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro kwa tuhuma za kuhusika na njama za kuvujisha mtihani wa kuhitimu elimu ya Msingi uliofanyika hivi karibu.

Miongoni mwa watuhumiwa hao ni walimu watano na mlinzi mmoja waliokuwa wakisimamia mtihani huo katika Shule ya Msingi Kambala iliyopo Wilayani Mvomero.

Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro (SACP) Fortunatus Musilimu, amewataja watuhumiwa hao ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kambala, Juliana Thomas; Msimamizi Mkuu wa Mtihani, Antonia Pastory; Mwalimu wa Doma Secondary; mtoto Francis, Mwalimu wa Shule ya Msingi Kinda, mwalimu Dorine James wa Shule ya Msingi Madizini, mwalimu Habibu Hango na mlinzi wa kituo hicho cha mitihani Mohammed Bajuka.

Kamanda Muslimu amedai kuwa watuhumiwa hao walikubaliana endapo mpango huo ungekamilika wangekabiziana shilingi laki mbili.