Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 21Article 558808

Habari za Mikoani of Tuesday, 21 September 2021

Chanzo: Channelten

Walimu wafanyia kazi chini ya mti

Walimu Walimu

Waalimu katika shule ya Sekondari Gichemeda Kata ya Magugu wilayani Babati wanalazimika kufanya shughuli zao chini ya Mti baada ya ofisi na Nyaraka zao kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo pamoja na baadhi ya Nyaraka za fedha.

Walimu Shuleni hapa wanafanya kazi zao hapa lakini watalazimika kuandaa upya maandalio ya kufundisha kutokana na kuteketea kwa Moto.

Kabla ya Moto kuleta madhara makubwa zaidi ulifanikiwa kudhibitiwa na wananchi wa kijiji cha Gichemeda.

Lakini kwanini wamekuwa wepesi kujitokeza kudhibiti Moto huo?

Kutokana na kupoteza Nyaraka zote muhimu ikiwemo andalio la kufundishia waalimu Shuleni hapa wanashauri njia mbalimbali zianze kutumika rasmi kama njia za kuhifadhi Nyaraka mashuleni kuokoa hasara inayojitokeza pindi yanapotokea majanga.