Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 23Article 573715

Habari Kuu of Tuesday, 23 November 2021

Chanzo: millardayo.com

Waliofanikisha kukamatwa magaidi kulipwa

Waliofanikisha kukamatwa magaidi kulipwa Waliofanikisha kukamatwa magaidi kulipwa

Serikali ya Kenya imesema inafanya uhakiki ili kulipa fedha kwa Mtu au Watu waliofanikisha kupatikana kwa Wafungwa watatu ambao walihukumiwa kwa Ugaidi na kufanikiwa kutoroka kwenye Gereza lenye ulinzi mkali la Kamiti nchini Kenya.

Kenya imesema kwakuwa ilitangaza dau waliojitokeza kusema wamefanikisha ni wengi na kusema wanahakiki ili wawalipe wale wanaostahili bila upendeleo huku wakisisitiza kuwa wataficha majina ya Watu hao kwa usalama wao, Wafungwa hao walikamatwa Msitu wa Enzio, Kaunti ya Kitui baada ya Raia kutoa taarifa kwa Polisi.

Itakumbukwa Serikali ya Kenya ilitangaza kuwa atakayefanikisha kupatikana kwa Wafungwa watatu wa Ugaidi waliotoroka Gerezani nchini humo atapatiwa Milioni 60 za Kenya ambazo ni sawasawa na zaidi ya Bilioni 1.2 za Kitanzania.