Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 24Article 553486

Uhalifu & Adhabu of Tuesday, 24 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Waliokamatwa na kilo 10 za Heroin wafikishwa Kisutu

Dawa za kulevya Dawa za kulevya

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewafikisha mahakamani watu watatu na kuwasomea shtaka la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine kiasi cha kilo 10 walizokamatwa nazo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Washtakiwa hao, Mohamed Yussuf, Sania Kombo na Nasri Khamis wote wakazi wa Zanzibar walifikishwa mahakamani hapo leo na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Ashura Mnzava mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Joseph Luambano.

Mnzava alidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo aliomba tarehe nyingine ya kutajwa kesi hiyo

Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Septemba 7, 2021 na washtakiwa walipelekwa mahabusu kwa kuwa shtaka linalowakabili halina dhamana.