Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 13Article 585352

Habari Kuu of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Waliokufa kwa Ajali Simiyu Wafikia 15

Waliokufa kwa Ajali Simiyu Wafikia 15 Waliokufa kwa Ajali Simiyu Wafikia 15

IDADI ya vifo vilivyoyokana na ajali iliyohusisha gari ya wanahabari ma Toyota Hiace imefikia 15 baada ya majeruhi mmoja aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Kanda ya Bugando kufariki dunia wakati akipatiwa matibabu.

Akitoa ripoti ya maendeleo afya ya majeruhi wa ajali hiyo kwa Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando, Dk Fabian Massaga amesema hospitali hiyo ilipokea majeruhi sita wa ajali hiyo ambapo mmoja amefariki (bila kumtaja jina), wanne wanaendelea na matibabu huku mmoja akiwa ameruhusiwa baada afya yake kutengemaa.

Dk Massaga amesema majeruhi hao wanne wanasubiria huduma ya matibabu ya upasuaji wa kibingwa unaotarajiwa kufanyika kuanzia kesho Alhamisi Januari 13, 2022.

"Hali za majeruhi mpaka sasa ni nzuri ikilinganishwa na jana walipofikishwa hapa, tunao wagonjwa wanne wanaosubiria upasuaji wa kibingwa wakiwemo waandishi wa habari ambao tunaamini baada ya matibabu hayo kukamilika watarejea kwenye utimamu wao," amesema Dk Massaga.

Naye Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel ameiagiza hospitali hiyo kuhakikisha inasimamia huduma ya matibabu kwa majeruhi hao ili wapone na kujuika na familia zao.

"Serikali itaendelea kufanya ufuatiliaji wa karibu wa hali za majeruhi hawa lengo ni kuhakikisha kwamba kila mmoja aliyejeruhiwa anapatiwa matibabu stahiki na anapona na kuendelea na shughuli zake.

Naye majeruhi, Vanny Charles ameishukuru Serikali na hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando kwa kumpatia huduma ya matibabu huku akidai kwamba hali ya afya yake imeanza kuimarika.