Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 15Article 585970

Habari Kuu of Saturday, 15 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Wanafunzi 10 Bora Kidato cha Nne

Wanafunzi 10 Bora Kidato cha Nne Wanafunzi 10 Bora Kidato cha Nne

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) leo Jumamosi, Januari 15, 2022 limetangaza matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne uliofanyika Novemba 2021.

Matokeo hayo yametangazwa na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde ambapo pia, baraza hilo limetangaza matokeo ya mitihani ya upimaji wa kitaifa ya darasa la nne na kidato cha pili 2021.

Akitangaza matokeo hayo, Dkt. Msonde amesema watahiniwa wa Shule 422,388 (87.30%) kati ya Watahiniwa 483,820 wamefaulu Mitihani yao ongezeko la ufaulu ni 1.46% ikilinganishwa na mwaka 2020.

Dkt. Msonde ametangaza watahiniwa 10 bora wa kidato cha nne ambao ni:
1. Consolata Prosper Luguva – St. Francis Mbeya
2. Butoi Ernest Kangaza – St. Francis
3. Wllhemia Steven – St. Francis
4. Cronel John – St Francis
5. Merry George Ngoso – St Francis
6. Holly Beda Lyimo – Bright Future Girls
7. Brandina – St. Francis
8. Imamu Suleiman – Feza Boys
9. Mfalme Hamis Madili – Ilboru
10. Clara Straton – St. Francis