Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 26Article 544435

Habari za Afya of Saturday, 26 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Wananchi wakosa huduma kisa nesi kuwa mjamzito

Wananchi wakosa huduma kisa nesi kuwa mjamzito Wananchi wakosa huduma kisa nesi kuwa mjamzito

Wananchi wameeleza kuwa wakati mwingine hufungwa  kwa wiki nzima hali ambayo wameeleza husababisha matukio ya wajawazito kujifungulia nje ya zahanati hiyo.

Kufungwa kwa zahanati hiyo inayotajwa kutegemewa na zaidi ya wananchi elfu 20 kunatokana na kuwa na mtoa huduma mmoja baada ya wapili kuwa katika likizo ya uzazi hali mbayo inamlazimu afanye majukumu ya kuhudumia wananchi peke yake na majukumu ya kiofisi ikiwemo kwenda katika mafunzo au kupeleka chanjo katika maeneo mengine ya mbali.

Magreth Ngw'endesha akielezea juu ya adha hiyo amesema kwa sasa klinik ya mama na mtoto haina ufanisi kwani wamekuwa wakitumia umbali mrefu kuendesha baiskeli ili kufika kupata huduma lakini wanakuta pamefungwa.

"Kwakweli hawa wanatunyanyasa ninaendesha baiskeli nikiwa nimebeba watoto kwa zaidi ya saa nzima lakini hii ni awamu ya tatu nakuta zahanati imefungwa"Amesema.

Mtoa huduma ngazi ya jamii Kalimba Sadick alipohojiwa na Nipashe mara baada ya kukuta zahanati ikiwa imefungwa alisema tangu June 22 siku ya jumatatu muuguzi alienda halmashauri kushughulikia suala la chanjo na amewataarifu wawaambie wananchi warudi June 30 atakaporejea.

"Ukihesabu inakuwa zaidi ya wiki hii ni hatari inayohitaji kushighulikiwa haraka"anasema.

Wanaeleza upungufu wa watumishi umekuwa ukisababisha wasipate muda wa kupewa elimu ya masuala mbalimbali ya afya ya uzazi ikiwemo matumizi ya uzazi wa mpango kwani mtoa huduma huyo huwa kwenye harakati za kuhudumia makundi mengine.

Akieleza mpango wa serikali wa kuwasaidia wananchi hao  mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Uvinza Weja Ng’ollo amesema tayari serikali imetenga shilingi milioni 50 za uboreshaji wa huduma katika eneo hilo upande wa miundombinu  na imo miongoni mwa zitakazo ongezewa watumishi.