Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 22Article 573586

Siasa of Monday, 22 November 2021

Chanzo: Nipashe

Wananchi watakiwa kupaza sauti viongozi wasipotekeleza wajibu wao

Wananchi watakiwa kupaza sauti viongozi wasipotekeleza wajibu wao Wananchi watakiwa kupaza sauti viongozi wasipotekeleza wajibu wao

WANANCHI wametakiwa kupaza sauti na kuishauri serikali pale wanapoona kuna maswala hayaendi vizuri katika maeneo yao ikiwemo baadhi ya watumishi waliojisahau na wasio tekeleza wajibu wao.

KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI CCM SHAKA HAMDU SHAKA.

Akizungumza na waandishi wa habari Leo Novemba 21, 2021 mara baada ya kukagua baadhi ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya Tanganyika mkoani Katavi Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Shaka Hamdu Shaka amesema niwajibu wa wananchi kuikumbusha serikali na kutoa kero zao. Amesema wao kama chama pamoja na kukagua utekelezaji wa irani pia wanakagua uimara wa chama katika maeneo mbalimbali kwa kukutana na kuzungumza na wanachama katika mashina yao.

Shaka amesema mikopo inayotolewa na Halmashauri kupitia vikundi kwa vijana na wanawake wahakikishe wanawapa kipaumbele vina waliohusika na ujenzi wa hospitali ya Ikola waweze kununua vifaa vya kazi ambavyo wameomba serikali iwasaidie.

"Hawavijana lazima wajengewe uwezo na muwape kipaumbele kama wamefanya kazi kubwa kama hii kwa uaminifu mkubwa lazima serikali muangalie ni jinsi gani ya kuwashika mkono maana msipofanya hivyo hawavija wachapakazi tutawapoteza, "amesema Shaka.

Hata hivyo Shaka ameahidi kujitolea kuwa mlezi na muangalizi wa kikundi cha vijana hao kwa kuwafatilia kwa ukaribu na kuwa bega kwa bega na wao ili iwe kama mfano kwa maeneo mengine huku akiamini vijana hao wakishikwa vizuri ipo siku watapewa mradi mkubwa kitu ambacho kitaepusha gharama kubwa ya kutumia mafundi wa njee.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu ameahidi kuyafanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa ikiwemo kusimamia vijana hao wapate mashine ya kuchanganya zege hiyo ni baada ya kutoa matatizo yanayo wakabili.

Hatahivyo ameahidi kutatua kero ya wakulima waliouza pamba na hadi sasa hawajalipwa pesa zao kwa kuzichukulia hatua Amcos zote zilizo husika na kutowalipa wakulima katika wilaya hiyo.