Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 31Article 554626

Habari za Mikoani of Tuesday, 31 August 2021

Chanzo: Jamii Forums

Wananchi wavamia nyumba ya mtu kuchimba dhahabu

Wananchi wavamia nyumba ya mtu kuchimba dhahabu Wananchi wavamia nyumba ya mtu kuchimba dhahabu

Watu zaidi ya 6,000 wamevamia nyumba ya Mwanakijiji mmoja wa Kijiji cha Nyambogo, Kata ya Nyakafuru, Wilayani Mbogwe baada ya kujua kuwa kuna madini ya dhahabu.

Eneo hilo lilibainika kuwa na dhahabu baada ya Mwanakijiji huyo kukuta mwamba unaosadikiwa kuwa na dhahabu alipokuwa akichimba choo, ambapo alikwenda kuchenjua na kupata dhahabu.

Baada ya tukio hilo aliendelea kuchimba dhahabu katika eneo hilo ambapo baadaye Wanakijiji waligundua na kuvamia eneo hilo. Uongozi wa Wilaya umejipanga kutembelea eneo hilo ili kulitolea majibu.