Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 30Article 554428

Habari Kuu of Monday, 30 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Wapangaji nyumba za Serikali watakiwa kulipa madeni yao

Wapangaji nyumba za Serikali watakiwa kulipa madeni yao Wapangaji nyumba za Serikali watakiwa kulipa madeni yao

Shirika la Nyumba Zanzibar ZHC limeahidi kuendelea na zoezi na kufatilia na kuchukua hatua kwa wapanagaji wote walioshindwa kulipa kodi ya nyumba zinazomilikiwa na shirika hilo ikiwa ni pamoja na kuwahamisha katika makaazi hayo.

Aidha Shirika hilo limewataka wapangaji hao kulipa haraka madeni yao, huku lkibainisha kuwa takribani bilioni 2.5 hazijalipwa ikiwa ni hesabu ya nyumba zote zilizopo Unguja na Pemba na kusema kuwa zoezi la awali la ukusanyaji lilipata kiasi cha bilioni 1.2.

wapangaji hao wametakiwa kuhakikisha wanalipa kodi kwa wakati ili kuiwezesha serikali kuzifanyia matengenezo nyumba hizo.