Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 31Article 554599

Habari Kuu of Tuesday, 31 August 2021

Chanzo: eatv.tv

Wapangaji watakiwa kuwashtaki wenye nyumba wakaidi tozo ya kodi ya jengo

Wapangaji watakiwa kuwashtaki wenye nyumba wakaidi tozo ya kodi ya jengo Wapangaji watakiwa kuwashtaki wenye nyumba wakaidi tozo ya kodi ya jengo

Afisa Msimamizi wa Kodi mkoa wa Kinondoni Mercy Macha, amesewataka wapangaji ambao wenye nyumba wao wanakataa kuwarejeshea pesa wanazokatwa wanaponunua LUKU kwa ajili ya kulipia kodi ya majengo basi wawasilishe malalamiko yao kwa Meneja TRA mkoa husika.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 30, 2021, wakati akizungumza kwenye kipindi cha Supa Breakfast ya East Africa Radio.

"Hadi sasa kuna wenye nyumba wameonesha ushirikiano, lakini kama itatokea kuna mpangaji ambaye mwenye nyumba amekataa kumrejeshea pesa yake iliyokatwa kwenye LUKU kutokana na kodi ya majengo atuandikie barua au afike kwa Meneja TRA wa mkoa husika na yeye atamuita mwenye nyumba,” amesema Mercy Macha