Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 23Article 559291

Habari Kuu of Thursday, 23 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Wapenzi Wafunga Ndoa Wodini

Maharusi wakifunga ndoa. Maharusi wakifunga ndoa.

Kijana Augustine Makule na Mpenzi wake Rose Kimaro wamefunga ndoa wodini jijini Dodoma kufuatia ajali ya bodaboda aliyopata bwana harusi siku mbili kabla ya harusi yao.

Ajali hiyo ya pikipiki iliyotokea eneo la Zuzu Dodoma na kusababisha Agustino kukatwa mguu wake wa kulia na vidole vitatu vya mguu wake wa kushoto.

Lakini licha ya maumivu makali aliyokuwa nayo akiuguza majeraha wodini, waliamua kuendelea na ratiba yao ya ndoa kama ilivyokuwa imepangwa awali ambapo waliamua kufungia ndani ya wodi.

Pole na hongera sana kwa Augustine na Rose.