Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 27Article 540112

xxxxxxxxxxx ya

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Warundi Wauza Alkasusu Kortini Kisutu

RAIA 29 wa Burundi wanaodaiwa kuuza kahawa aina ya alkasusu na kahawa ya kawaida, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakituhumiwa kuingia nchini na kuishi kinyume cha sheria.

Kati yao, washtakiwa 13 wamekiri makosa wakiwamo watoto wanne na wengine 16 wamekana mashtaka hayo. Washtakiwa wamesomewa mashtaka yanayomkabili mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, jana.

Wakili wa Serikali, Godfrey Ngwijo, aliwataja washtakiwa hao kuwa ni pamoja na Kassim Mkoko, Elias Shadra, Hilary Lozo, Richard Dismas, Ntahondereye Reverie, Baraka Yosam, Meraki Noah, Robert Lazaro, Samson Erick, Kazimana Aimable, John Ayoub, Donald Kasendi, Elias Jonias, Shabani Makangila, Minani Festo, William Aston, Salasio Jeradi, Niubuntu Baraka, Majaliwa Novatus, Nionkuru Odasi, Boniface Chubwa.

Wengine ni Shabani Mussa, Jedio Misigo, Kuruwa Cpliano, Shadrack Bagoye, Daud Yokonia, Steven Mkonu, Asheri Selekela na Mussa John. Washtakiwa ambao ni watoto chini ya miaka 18, wamewekwa chini ya Ustawi wa Jamii.

Mahakamani huko washtakiwa wote walisomewa mashtaka mawili ya kuingia nchini bila viza na lingine la kuishi nchini bila viza. Wakili Godfrey alidai washtakiwa walitenda makosa hayo Mei 25, mwaka huu, maeneo mbalimbali ya Kariakoo na Jangwani.

Wakili wa Serikali, Godfrey, aliomba mahakama iahirishe kesi ili ipangwe tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali.

Hakimu Shaidi alikubali kuahirisha kesi hiyo hadi Juni, Mosi mwaka huu kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa waliokiri na kuwapa muda washtakiwa waliokana, kutafakari na kufika na vibali vilivyowaruhusu kuishi nchini.

Kesi itakuja Juni, Mosi mwaka huu na washtakiwa wote walipelekwa mahabusu isipokuwa watoto ambao walikabidhiwa kwa Idara ya Ustawi wa Jamii hadi tarehe ya kesi ijayo.

Join our Newsletter