Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 20Article 543568

Habari za michezo of Sunday, 20 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Wasanii kutumbuiza UMITASHUMTA Mtwara

Wasanii kutumbuiza UMITASHUMTA Mtwara Wasanii kutumbuiza UMITASHUMTA Mtwara

Hayo yamesema na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Hassan Abbasi, huku akisema kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imewekeza kikamilifu na inaendelea kutoa kipaumbele kwenye Sekta ya Sanaa hivyo anawaalika wadau mbalimbali kuja kushuhudia burudani zitakazotolewa na wasanii.

Amesema wakati wa ufunguzi wa UMITASHUMTA wasanii mbalimbali wakiongozwa na Ibrah kutoka Konde Gang, Beka Flavour, Peter Msechu na Linah Sanga, pia msanii maarufu wa Singeli Dulla Makabila na Mfalme wa taarabu Mzee Yusuf, walitoa burudani ambapo amesema katika awamu hii vikundi mbalimbali vya ngoma za asili, kwaya na Sanaa nyingine vimealikwa ili kuongeza hamasa na kutoa burudani wakati mashindano hayo yanaendelea.

Aidha, amesema kwenye mashindano hayo Serikali imealika vilabu, vyama, na mashirikisho mbalimbali kuona vipawa na vipaji vya wanamichezo hao chipukizi kutoka Tanzania bara na visiwani ili waweze kuwaendeza.