Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 06Article 583636

Habari Kuu of Thursday, 6 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Wasioandikisha Watoto Kufikishwa Mahakamani, Walioacha kwa Mimba Warudi

Wasioandikisha Watoto Kufikishwa Mahakamani, Walioacha kwa Mimba Warudi Wasioandikisha Watoto Kufikishwa Mahakamani, Walioacha kwa Mimba Warudi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu amewataka wazazi wote ambao watoto wao wamefaulu kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu lakini hawatokwenda kwenye shule za Serikali hasa shule maalum, watoe taarifa kwa kujaza fomu maalumu kuwawezesha wale waliokosa nafasi kwenye shule hizo kupata kukiwa na nafasi.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Alhamisi Januari 6, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari akitoa taarifa ya maandalizi na mapokezi ya wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na darasa la awali, la kwanza na kidato cha kwanza mwaka huu.

Aidha, Waziri Ummy amesema wazazi ambao watashindwa kupeleka watoto Shuleni watachukuliwa hatua kali ikiwemo kuwafikisha Mahakamani.

"Ninaitaka Mikoa, isisite kuwachukulia hatua wazazi au walezi wowote ambao wanawaficha watoto wenye umri wa kwenda Shule. Na Lazima wawachukulie hatua kali kwa mujibu wa sheria na taratibu.

"Na tunaitaka Mikoa ituletee taarifa ya hali ya uandikishaji kila Ijumaa ya mwisho wa wiki kuanzia sasa... Kesho baada ya saa 10 Jioni, naielekeza mikoa kuniletea taarifa ya hali ya Uandikishaji wa watoto wa darasa la awali na darasa la kwanza.

"Maafisa Elimu wa Wilaya na maafisa Elimu wa Mikoa, watawajibika kwa suala lolote ambalo tutalibaini kwamba Shule zilizo katika Wilaya zao zinatoza ada na michango kwa ajili ya wanafunzi wanaoandikishwa darasa la awali na darasa la Kwanza.

"Nitoe wito pia kwa wakuu wa Mikoa kuhakikisha kuwa wanafunzi walioacha shule kwasababu mbalimbali ikiwemo ujauzito wanarejea shuleni kwa kuzingatia miongozo mbalimbali ya Elimu ikiwa ni pamoja na waraka wa Elimu Namba 3 wa mwaka 2021," amesema Ummy Mwalimu.