Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 31Article 554575

Uhalifu & Adhabu of Tuesday, 31 August 2021

Chanzo: Mwananchi

Wasiojulikana waua mwanamke Moshi

Marehemu, Elice Matafu Marehemu, Elice Matafu

Elice Matafu, Mkazi wa Kijiji cha Mrimbo Uuwo, Kata ya Mwika Kaskazini, Wilaya ya Moshi ameuawa kwa kukatwa shingo na watu wasiojulikana nyumbani kwake, usiku wa saa 2.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kuuawa kwa mwanamke huyo na amesema mauaji hayo yanaviashiria vya visasi ambapo tayari anashikiliwa kijana mmoja kwa mahojiano zaidi.

"Ni kweli huyu mwanamke ameuliwa nyumbani kwake usiku kwa kukatwa shingo na inaonekana kuna viashiria vya visasi, tayari tunamshikilia kijana mmoja kwa mahojiano zaidi,"amesema Kamanda Maigwa.

Kamanda Maigwa amesema wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini hasa chanzo cha mauaji hayo.