Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 26Article 574099

Habari Kuu of Friday, 26 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Wasumbufu wa Kurejesha Mikopo ya Benki, Kesi za Tsh Tril 1.2 Zaunguruma

Nsekela Nsekela

MWENYEKITI wa Umoja wa Benki Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema kesi zinazohusu mikopo yenye thamani ya zaidi ya Sh trilioni 1.2 ambazo haijarejeshwa zinaendelea katika hatua mbalimbali za maamuzi.

Amesema mikopo inayochelewa kurejeshwa inatoa changamoto kwa taasisi za kifedha kuongeza mikopo na mitaji.

Akiongea katika Mkutano wa 20 wa Taasisi za Fedha nchini, ulioandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania, BoT, Nsekela amesema “bado watanzania wachache wanaokopeshwa hawarejeshi sawasawa.”

Nsekela amepongeza Benki Kuu kwa kutekeleza sera mbalimbali ambazo zitaleta chachu ya kufanya mabenki kupunguza riba. Hadi sasa benki zimekuwa zikifanya utaratibu wa kuja na taarifa mbalimbali za kupunguza riba katika mikopo watakayo toa.

“Hivi karibuni utaanza kuona benki zikiaza kutangaza kupunguza riba hizo,” alisema wakati wa mkutano uliohudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan.