Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 15Article 586057

Habari Kuu of Saturday, 15 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Watahiniwa 214 wafutiwa matokeo

Watahiniwa  214 wafutiwa matokeo Watahiniwa 214 wafutiwa matokeo

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza kufuta matokeo yote ya watahiniwa 214 waliofanya udanganyifu katika upimaji kitaifa wa darasa la nne, kidato cha pili, kidato cha nne na mtihani wa maarifa (QT).

Katika matokeo ya yaliyotangazwa leo Januari 15, 2022 na Katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk. Charles Msonde yameonesha kuwa kati ya watahiniwa waliobainika kufanya udanganyifu, watahiniwa 83 ni wa Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne (SFNA).

“Watahiniwa 27 ni wa Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili (FTNA), 102 ni wa Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Watahiniwa 02 ni wa Mtihani wa Maarifa(QT).

Akizungumzia hilo Dk Msonde amesema Baraza limeamua kufuta matokeo hayo kwa mujibu wa Kifungu cha 5 (2) (i) na (j) cha sheria ya Baraza la Mitihani sura ya 107 kikisomwa pamoja na Kifungu cha 30(2) (b) 2016 cha Kanuni za Mitihani.

Aidha amesema umatokeo ya watahiniwa 555 yamezuiliwa kutokana na watahiniwa hao kupata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya upimaji/mtihani kwa masomo yote au idadi kubwa ya masomo.

“Watahiniwa husika wamepewa fursa ya kufanya upimaji/mtihani kwa masomo ambayo hawakuyafanya kwa sababu ya ugonjwa mwaka 2022 kwa mujibu wa Kifungu cha 32(1) cha Kanuni za Mitihani.

“Kati ya watahiniwa waliopewa fursa ya kurudia upimaji/mitihani yao mwaka 2022, watahiniwa 198 ni wa Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili (FTNA) na 357 ni wa Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE).

Matokeo kidato cha nne haya hapa

Pamoja na mambo mengine amesema matokeo ya Mtihani wa Maarifa (QT) takwimu zinaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 4,763 sawa na asilimia 57.23 ya watahiniwa 8,324 wenye matokeo ya Mtihani wa Maarifa (QT) wamefaulu.

“Mwaka 2020 jumla ya watahiniwa 4,446 sawa na asilimia 55.19 walifaulu mitihani wa Maarifa (QT), hivyo ufaulu wa Mtihani wa Maarifa (QT) umepanda kwa asilimia 2.04,” amesema.