Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 15Article 542707

Habari Kuu of Tuesday, 15 June 2021

Chanzo: eatv.tv

Watanzania tuanze kuvuna majia ya mvua- Rais Samia

Rais Samia Rais Samia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametoa wito kwa Watanzania kuanza utamaduni wa kuvuna maji ya mvua kwani itasaidia kupunguza na ikiwezekana kumaliza tatizo la maji nchini.

Submitted by Elbogast on Jumatatu , 14th Jun , 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi wa Mkuyuni na Butimba mkoani Mwanza.

Rais Samia maesema hayo wakati wa ufunguzi wa Mradi wa Maji Misungwi mkoani Mwanza leo, Juni 14, 2021 ambapo amewataka wananchi wa Misungwi kuitunza miundombinu ya maji.

"Nitoe wito kwa Watanzania kuanza utamaduni wa kuvuna maji ya mvua kwa kujenga mabwawa, matenki au visima kwenye maeneo yetu, nchi yetu imebahatika kupata kiasi kikubwa cha mvua ila maji hutiririka baharini, tukiweza kuvuna maji ya mvua tatizo la maji litapungua au kumalizika nchini," amesema Rais Samia.

Awali akimkaribisha Rais Samia Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso, amesema wizara yake itahakikisha maji yanapatikana kwa wananchi kwani maji hayana mbadala nakuahidi kuwachukulia hatua wanaoshiriki kuwarubuni wananchi.

 "Asitokee mtu kwa makusudi mradi ambao umetumia gharama nyingi mtu anataka kuunganishiwa maji mnamtajia gharama kubwa, niwahakikishie hata uwe na mapembe marefu kiwango gani tutayakata ili kuwanusuru Wanamisungwi waweze kupata maji safi," amesema Waziri Aweso.

Leo ikiwa ni muendelezo wa ziara ya ya siku tatu ya Mhe Rais Samia mkoani Mwanza amezungumza na wananchi wa Butimba, amekagua ujenzi wa daraja la Magufuli la Kigongo Busisi pamoja na kuzindua mradi wa maji wa Misungwi huku akitarajia kuzindua mradi wa treni ya mwendo kasi SGR mkoani humo.