Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 28Article 540268

Habari Kuu of Friday, 28 May 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Watanzania wahimizwa kukienzi Kiswahili

Watanzania wahimizwa kukienzi Kiswahili Watanzania wahimizwa kukienzi Kiswahili

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamaganda Kabudi amehimiza Watanzania wajifunze Kiswahili, wakienzi na waache kuiharibu lugha hiyo kwani Tanzani si nchi pekee inayoitumia.

Alisema hayo jana jijini Dodoma wakati wa kikao kazi cha wakurugenzi wa idara na vitengo vya sheria vya wizara na serikali kueleza hatua zilizofikiwa katika kazi ya kuzitafsiri sheria.

“Sisi si wazungumzaji pekee wa Kiswahili, nchi za Afrika Mashariki zote zinazungumza Kiswahili, Madagascar, Comoro, Congo. Tumeacha kujifunza Kiswahili sanifu kwa vile tunajua tumezaliwa na Kiswahili na tunakijua sana,” alisema Profesa Kabudi.

Alisema mauzo ya kamusi ya Kiswahili nchini Kenya ni maradufu ya mauzo ya hapa nchini na kuwataka Watanzania waanze kutumia kamusi na vitabu ili kuijua vizuri lugha hizyo.

‘Kuna kituo cha televisheni nchini Kenya watangazaji wake wanazungumza lugha Kiswahili chenye ladha,” alisema.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju alisema sheria kuu 449 zote zitawekwa kwa lugha ya Kiswahili.

“Misamiati huwa hailingani, maneno huwa na matumizi tofauti, kutakuwa na kikosi kazi cha kupokea rasimu baadaye zoezi hilo litaendele,” alisema.

Profesa Kabudi alisema kazi ya kutafsiri sheria katika lugha ya Kiswahili itakuwa endelevu na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano ilifanya uamuzi sahihi kuifanya lugha hiyo kuwa ya msingi na mama katika utoaji haki mahakamani.

”Kazi ya kutafsiri sheria kwa lugha ya Kiswahili itakuwa endelevu kwani linahitaji umakini na maandalizi ya kutosha, wadau wote wakiwemo wanazuoni, viongozi wa dini wanatakiwa kuunga mkono juhudi za serikali juu ya matumizi ya Kiswahili katika utoaji haki,” alisema.

Join our Newsletter