Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 11Article 584854

Habari Kuu of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Watu 14 wafariki ajali ya gari Simiyu

Watu 14 wafariki ajali ya gari Simiyu Watu 14 wafariki ajali ya gari Simiyu

Watu 14 wamefariki dunia baada ya gari la waandishi wa habari iliyokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (RC), Robert Gabriel kugongana na gari ya abiria Hiace katika eneo la Nyamikoma wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu akiwa eneo la tukio, Mkuu wa Wilaya ya Busega (DC), Gabriel Zakaria amethibitisha kutokea vifo hivyo.

Amesema kati ya vifo hivyo kuna vifo vya waandishi wa habari wanne na dereva wa waandishi na watu wengine sita walifariki papo hapo

“Ni kweli ajali hiyo imetokea, watu 11 wamefariki kwenye eneo la tukio wakiwemo waandishi wa habari 4 na dereva na wengine sita waliokuwa kweneye gari lingine” amesema Zakaria na kuongeza

“Dakika chache majeruhi waliopelekwa kwenye kituo cha afya cha Nasa watatu walifariki, wakiwemo wale waandishi wa habari waliokuwa kwenye msafara”