Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 24Article 553468

Uhalifu & Adhabu of Tuesday, 24 August 2021

Chanzo: MillardAyo

Watu 17 washikiliwa kwa tuhuma za utapeli kwa njia ya Madini feki

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Muliro Jumanne Muliro. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Muliro Jumanne Muliro.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linawashikilia Watu 17 kwa tuhuma mbalimbali za kijinai ikiwemo utapeli wa fedha kwa kutumia madini feki.

Hatua hiyo inatokana na Oparesheni inayoendeshwa na Jeshi hilo ikiongozwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Muliro Jumanne Muliro.

Kamanda Muliro amesema Oparesheni hiyo inalenga kuzuia vitendo vya kihalifu na kuwakamata wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.

"Oparesheni hii inahusisha vikosi vya mbwa na farasi,askari wa miguu,doria za magari na pikipiki imeleta mafanikio ikiwemo tukio la kukamatwa kwa Watuhumiwa 13 wa makosa yakujipatia pesa kwa njia za udanganyifu (utapeli) wa madini bandia” ——— Muliro.