Uko hapa: NyumbaniHabari2021 07 13Article 546901

Uhalifu & Adhabu of Tuesday, 13 July 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Watumishi sita wahusishwa ubadhirifu milioni 520/- za NHIF Kilimanjaro  

Watumishi sita wahusishwa ubadhirifu milioni 520/- za NHIF Kilimanjaro    Watumishi sita wahusishwa ubadhirifu milioni 520/- za NHIF Kilimanjaro  

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imebaini uwepo wa ubadhirifu wa zaidi ya Sh milioni 520 katika miamala ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Kilimanjaro.

Ubadhirifu huo unadaiwa kuhusisha watumishi sita kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda KCMC pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mawenzi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dk Godwin Mollel mara baada ya kikao kazi na viongozi wa mkoa, na kudai kuwa ukaguzi maalumu uliofanyika unaitaja Hospitali ya KCMC kuongoza kwa ubadhirifu wa shilingi milioni 245 ikifuatiwa na Hospitali ya Saint Joseph, shilingi milioni 46, pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi shilingi milioni 38, ambapo watumishi hao wameghushi nyaraka na kujipatia fedha hizo kinyume na sheria.

Dkt. Mollel ameongeza kuwa ubadhirifu huo pia umefanywa na baadhi ya watumishi kwa kushirikiana na baadhi ya maduka ya dawa za binadamu ambapo uchunguzi unaendelea zaidi ili kubaini wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai ameviagiza vyombo vya usalama kuwakamata watumishi wote waliohusika kufanya ubadhilifu huo pamoja na kuhakikisha fedha hizo zinarejeshwa.