Uko hapa: NyumbaniHabari2021 10 01Article 560647

Habari Kuu of Friday, 1 October 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Watumishi waidai halmashauri Tsh. Bilioni 1.6/- za uhamisho

Watumishi waidai halmashauri Tsh. Bilioni 1.6/- za uhamisho Watumishi waidai halmashauri Tsh. Bilioni 1.6/- za uhamisho

HALMASHAURI ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, inadaiwa Sh bilioni 1.6 ikiwa ni fedha za malimbikizo ya uhamisho wa watumishi.

Hayo yameelezwa kwenye kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kilichoitishwa kufunga hesabu za mwaka wa fedha ulioisha Juni 30, 2021.

Mkurugenzi wa Halmashauri, Lino Mwangeni, alisema kwamba madeni ya watumishi hao yatalipwa kwa kadri ofisi yake inavyopata fedha, kwani kwa sasa halmashauri haina fedha.

Aliwataka madiwani kuchangia taarifa hiyo ili waweze kuondoa changamoto zilizomo zinazosababisha hati chafu.

Akichangia hoja, Diwani wa Kata ya Nyankende, Doa Limbu, alisema ni vyema mchakato ufanyike ili watumishi hao walipwe stahiki zao.

"Watumishi wanadai malimbikizo ya uhamisho ni haki yao walipwe na hili deni lao lipo kisheria na wakilipwa tunaweza kupunguza kwenye hoja za mkaguzi ambazo zimekuwa zikijirudia," alisema Limbu.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Gagi Lala, alisema malipo ya watumishi hao yapo kisheria hivyo ni vyema wakalipwa kupunguza hoja za mkaguzi.