Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 04Article 540898

Habari Kuu ya

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Wawekezaji wahimizwa kushirikiana na serikali

Wawekezaji wahimizwa kushirikiana na serikali Wawekezaji wahimizwa kushirikiana na serikali

WAWEKEZAJI katika sekta binafsi wamehimizwa kushirikiana kikamilifu na serikali ili kuleta maendeleo na kuinua fursa zaidi za uwekezaji nchini.

Aidha, miradi 40 kati ya 41 imeandaliwa na mamlaka za serikali kutoka sekta mbalimbali na mradi mmoja ukiwa na mwekezaji kutoka sekta binafsi.

Imefahamika kuwa, miradi hiyo 41 ipo katika hatua mbalimbali za maandalizi na itagharimu Sh 3,042,234.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba alibainisha hayo jijini Arusha wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango juu ya Ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP).

Katika ufunguzi huo, Tutuba alisema uwekezaji huo utasaidia kukuza uchumi wa nchi na kila mmoja kupata maendeleo.

Alisema kuna maeneo mengi ya uwekezaji hususan katika elimu, afya, mazingira na kuisisitiza sekta binafsi kubuni na kuwasilisha miradi yenye sifa za kipekee kwa mamlaka za serikali kwa utaratibu wa miradi inayoibuliwa.

Tutuba alisema serikali imeweka utaratibu ili kufanikisha malengo na mipango ya maendeleo ya nchi ikiwemo Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Miaka Mitano (2021/22 – 2025/26) na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kamishna wa Ubia Kati ya Serikali na Sekta Binafsi (PPP), Dk John Mboya, alisema utaratibu wa ubia ni njia muhimu na vyanzo mbadala vya kugharamia miradi ya maendeleo

Kwa mujibu wa Mboya, wadau 829 walipewa elimu ya ubia katika idara mbalimbali na mwaka 2020/21 elimu hiyo ilitolewa kwa watumishi 50.

Join our Newsletter