Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 13Article 551425

Habari za Mikoani of Friday, 13 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Waziri Apokelewa na Ndoo za Maji kichwani

Waziri wa Maji, Juma Aweso Waziri wa Maji, Juma Aweso

Waziri wa Maji, Juma Aweso, amepokelewa na wakina mama wenye ndoo za maji vichwani alipotembelea mradi wa Maji Nyarombo, Rorya Mkoani Mara.

Akiwa katika eneo la mradi huo, amemugiza Mkandarasi wa GAIMO CONSTRUCTION LTD anayetekeleza ujenzi wa miundombinu ya mradi huo wa Maji kufikisha maji katika Tanki la mradi ili wananchi waweze kupata huduma ya majisafi na salama ndani siku Saba (7)

"Nataka nikiondoka hapa Nyarombo na maji yawe yanapatikana, nikiondoka hapa jumatatu hizo milioni 80 nitakuwa nimezitoa, natoa dhamana kwamba Mh. Mbunge umeomba milioni 80 nitazitoa, hii yote ni kutimiza adhma ya Rais ya kumtua mama ndoo ya maji kichwani inatimilika. Mkandrasi na mtu wa umeme waje ofisini jumatatu, watueleze umeme unakamilika lini, sisi tunataka maji ndani ya siku ya siku saba"