Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 28Article 554104

Habari za Mikoani of Saturday, 28 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Waziri Aweso, atoa siku 30 maji yapatikane Handeni

Waziri wa Maji, Juma Aweso Waziri wa Maji, Juma Aweso

Waziri wa maji, Juma Aweso, ametoa siku 30 kwa watendaji wa Sekta ya Maji Handeni kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana na kuboresha uzalishaji ili wananchi wapate Maji.

Ametoa kauli hiyo mara baada ya kutembelea vyanzo na miradi ya maji wilayani Handeni.

Aidha, amemuagiza Mkurugenzi wa idara ya usambazaji maji na usafi wa mazingira kutoka wizara ya maji CPA, Joyce Msiru na timu ya wataalamu toka wizarani kubaki Handeni kuhakikisha wanakuja na mkakati mahususi wa kutatua kero ya upatikanaji wa huduma ya Maji Handeni Mjini ikiwa vyanzo vya Maji vipo.

Wakati huo huo Aweso amefanya mabadiliko ya kiutendaji na kuahidi kuleta nguvu mpya itakayoboresha eneo la uendeshaji na usimamizi ila kuleta mabadiliko Mji wa Handeni na viunga vyake.

Mwisho amesisitiza kuwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali imetenga zaidi ya Shilingi Bilioni 21 katika Mkoa wa Tanga ili kutekeleza miradi ya maji vijijini ikiwemo wilaya ya Handeni.