Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 07Article 555871

Habari Kuu of Tuesday, 7 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Waziri Aweso awataka wakala wa maji vijijini kufanya kazi kidigitali

Waziri Aweso awataka RUWASA kufanya kazi kidigitali Waziri Aweso awataka RUWASA kufanya kazi kidigitali

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, ameuelekeza uongozi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kuwa na mkakati wa kutumia vifaa vya kisasa katika utekelezaji wa miradi ya maji nchini.

Waziri Aweso amesema hayo wakati akipokea taarifa ya RUWASA kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji ya vijijini tangu ilipoanza kazi Julai 2019.Amesisistiza kuwa ni muhimu sana wakawa na vifaa vyao vya kisasa ili kurahisiasha utekelezaji wa miradi ya maji, ikiwa ni pamoja na kumaliza kwa wakati sambamba na kupunguza gharama kwa kuwatumia wakandarasi.

“Tunachohitaji ni kuona miradi inakamilika kwa wakati, Serikali ipo tayari kutoa fedha za kuhakikisha RUWASA inakuwa na vifaa vya kisasa kabisa,” Waziri Aweso amesema.

Wakati wa tukio hilo la upokeaji wa taarifa, Waziri huyo amemuelekeza Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Mhandisi Clement Kivegalo kufanya tathmini ya Wahandisi wa maji wa idara hiyo ili kujiridhisha na weledi na utayari wao wa kuwafikishia wananchi huduma ya majisafi.

“Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amedhamiria kwa dhati kumtua mwanamama wa Tanzania ndoo kichwani, sasa ni muhimu tukazingatia hili na Mhandisi asiyekuwa na uwezo wa kazi aondolewe tuwaache wenye uwezo,” Waziri Aweso amesisitiza