Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 26Article 553915

Habari za Mikoani of Thursday, 26 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Waziri Aweso azindua mradi wa maji wa Tsh. Biilioni 9

Waziri wa Maji, Juma Aweso Waziri wa Maji, Juma Aweso

Waziri wa Maji, Juma Aweso, amezindua mradi wa kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya Majisafi Jiji la Tanga awamu ya Pili wenye uliogharimu zaidi ya Bilioni 9 chini ya mpango wa Wizara ya Maji wa (OFF-OBA) kwa ufadhili wa Benki ya TIB, Uliogharimu zaidi ya bilioni 9 hadi kukamilika kwake.

Aidha mradi huo ambapo mradi utaweza kuongeza uzalishaji maji katika kituo cha Mowe kwa lita za ujazo 1000 kila siku.

Hata hivyo ameitaka Mamlaka ya maji jijini humo kuongeza uzalishaji wa huduma hiyo ili kuweza kukidhi mahitaji ya wananchi lakini pia kwa kuzingatia kuwa Jiji hilo lina viwanda vingi na vyote vinategemea maji kuendesha uzalishaji.

"Jiji la Tanga linauhitaji mkubwa wa Maji, tunaona uwekezaji mkubwa unafanyika jijini hapa kama wa bomba la mafuta, Tanga ni eneo la viwanda, hivyo tunawaomba Tanga- UWASA kuongeza uzalishaji utakaokidhi mahitaji, ili suala hili la maji lisiwe kikwazo" Waziri, Aweso

Aidha ameipongeza Mamalaka hiyo kwa kujitahidi kufikisha huduma ya maji pembezoni mwa Jiji hilo hasa maeneo ya Muheza na Mkinga , kwani hatua hiyo inatoa tafsri nzuri iliyowekwa na Wizara hiyo chini ya kauli mbiu ya Rais Samia ya "kumtua mama ndoo ya maji kichwani" inafikiwa kwa viwango na wakati sahihi.