Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 13Article 557251

Habari Kuu of Monday, 13 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Waziri Bashe apiga marufuku matumizi ya kamba za 'Naylon'

Hussein Bashe, Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, Naibu Waziri wa Kilimo

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussen Bashe, amepiga marufuku matumizi ya kamba za 'naylon' maarufu kama 'Manila' pamoja na gunia za aina hizo kutumika katika upakiaji wa mizigo nchini.

Ametoa marufuku hiyo leo Septemba 13,2021 wakati wa mkutano wake na wadau wa kilimo cha katani nchini, huku akiwaahidi wakulima hao kuwa kupitia Wizara watahakikisha wanadhibiti matumizi hayo.

"Nataka niwakikishie wakulima wa katani, tunaanza safari ya gunia za katani, nimewaagiza FRA ni marufuku kununua kamba za nailoni za kufungia magunia, Waziri ameshatupa muelekeo na tayari tumeanza kulifanyia kazi" Waziri Bashe

Aidha amesema kuwa Wizara hiyo itaendelea kuwasaidia wakulima hao kuongeza uzalishaji kwa kuwekeza kwenye maabara za uzalishaji wa katani ili kuweza kufikia malengo ya kutengeneza tani laki 120 kuweka pia amewataka halmashauri zote kutenga maeneo kwa ajili ya vitaru ili kuwapa wanachi miche hiyo bure.