Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 20Article 543547

Habari Kuu of Sunday, 20 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Waziri: Bodi ya walimu itaondoa ‘makanjanja’

Waziri: Bodi ya walimu itaondoa ‘makanjanja’ Waziri: Bodi ya walimu itaondoa ‘makanjanja’

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema Bodi ya Kitaalamu ya Walimu itaondoa ‘makanjanja.’

Amesema hayo jijini Dar es Salaam katika mkutano wa wadau wa elimu waliokuwa na jukumu la kutoa maoni kuboresha sheria na kanuni zinazounda Bodi ya Kitaalamu ya Walimu nchini.

Alisema bodi hiyo itasaidia kuwapata walimu wenye vigezo kwani na kuondokana na walimu wasiotimiza majukumu yao.

“Ndio hao walimu makanjanja, Bodi itakayoundwa itawaondoa hao walimu makanjanja, nilazima tuwe na walimu wenye viwango,” alisema.

Akaongeza: “Aprili 25, Rais Samia Suluhu alifanya kikao na viongozi wa wafanyakazi nchini suala la Bodi ya Kitaalamu liliibuka, siku ya Mei Mosi mwaka huu pale Mwanza, Rais Samia alizungumzia bodi hii ya kitaalamu na kutaka yafanyiwe kazi haraka tena alitumia neno ‘Mtoto akililia embe Mpe’ kikao cha leo ni utekelezaji,” alisema Ndalichako.

Alisema mwaka 2018, Bunge lilipitisha Muswada wa Sheria ya Kuunda Bodi ya Kitaalamu ya Walimu ya Tanzania, ambapo Wizara ya Elimu ilitunga kanuni za kuwezesha utekelezaji wa majukumu ya bodi hiyo baada ya kusainiwa kwa sheria hiyo.

“Baada ya kutungwa kanuni hizo, Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kilielezea kutoridhishwa na baadhi ya vipengele vya kanuni hizo, hivyo wizara imeona ni vema kuwashirikisha wadau na kuamua kuitisha kikao kitakachosikiliza maeneo ya Kanuni na Sheria za Bodi yanayoonekana yataleta changamoto katika utekelezaji,” alisisitiza Rais wa CWT, Leah Ulaya, aliishukuru serikali kwa kuitisha kikao hicho.

Alisema uanzishwaji wa bodi hiyo ni mzuri, lakini wanaona utekelezaji umeanza mapema kwani walimu wengi bado hawana uelewa wa kutosha kuhusu bodi hiyo.