Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 18Article 552208

Habari za Mikoani of Wednesday, 18 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Waziri Gwajima amtaja Mtendaji aliyezuia mtoto wa miaka 9 kwenda shule

Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima , ametuma salamu kwa Mtendaji wa kata Mkoani Mwanza, ambaye aliishi na mtoto mmoja aliyekoseshwa haki ya kwenda shule kwa muuguza bibi wakati watendaji hao wakiwepo katika eneo hilo.

Ametoa kauli hii wakati zikiwa zimepita siku kadhaa tangu taarifa ya mtoto huyo kusambaa katika mitandao na vyombo vya habari, huku watu wengi wakionesha kuguswa na hali ya mtoto huyo.

“Mwanza mwambieni, Mtendaji wa Mtaa, Kata, ambayo yupo mtoto aliyenyimwa haki ya kwenda shule, ana miaka tisa pamoja na akili yote hiyo haendi shulena watendaji wametulia tulia wanasubiri ndugu wajitokeze nakuja Mwanza"

Amewataka wananchi wote kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia pamoja na vitendo vyote vinavyo mnyima mtoto haki ya kupata elimu kwa usawa.