Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 13Article 551422

Habari Kuu of Friday, 13 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Waziri Liberata aongoza Mkutano SADC

Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 41 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC.

Katika mkutano huo Waziri Mulamula aliomgozana na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Adelardius Kilangi.

Kikao hicho cha Baraza la Mawaziri wa SADC kinafanyika hii leo Agosti 13,2021 katika jiji la Lilongwe nchini Malawi.