Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 31Article 554647

Siasa of Tuesday, 31 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Waziri Mambo ya Ndani kuitwa Kamati ya Maadili Sakata la Gwajima

Job Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania

Spika Job Ndugai amesema Vyombo vingine vya Serikali na Chama vinapaswa kumuwajibisha Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima kutokana na kauli zake

Amesema kama hatowajibishwa na akarudia makosa aliyokutwa nayo, Kamati ya Maadili ya Bunge italazimika kumuita Waziri wa Mambo ya Ndani na kumuhoji.

Pia Spika huyo, ameviijia juu vyombo vya Dola kwa kulega kuchukua hatua dhidi ya Mbunge huyo kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria aliofanya.