Uko hapa: NyumbaniHabari2021 10 07Article 561883

Habari za Mikoani of Thursday, 7 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Waziri Mku akataa kuzindua barabara Lindi

Waziri Mku akataa kuzindua barabara Lindi Waziri Mku akataa kuzindua barabara Lindi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambae siku zote pamoja na mambo mengine husifika kwa misimamo na uzingatiaji wa ubora wa miradi mbalimbali ya Serikali, leo akiwa katika siku ya Pili ya ziara yake Mkoani Lindi amegoma kuzindua barabara ya Liwale Mjini ya kilometa 1.2 kwa sababu haijawekwa taa za barabarani.

Amesisitiza kusema kuwa ujenzi huu umekwenda kinyume na makubaliano yaliyowekwa na Serikali, kwani mapango ni kujenga barabara za viwango vya lami zenye taa.

“Mkataba ni kujenga barabara za kiwango cha lami zenye taa, leo mnaniambia nizindue barabara haina taa, hii haijakamilika, leo sizindui sababu hamna taa, hayo ni maelekezo ya Rais Samia barabara ya kilometa 1.2 iwe na taa, siku yoyote nitakuja leo siwezi kuzindua” amesema Waziri Mkuu.

Taa za barabarani ni moja ya vitu muhimu vinavyopendezesha miji kama inavyoonekana kwenye Miji mbalimbali ikiwemo Lindi mjini kwenyewe ambako kumewekwa taa hizo ambazo licha ya kupendezesha mji, pia zinasaidia usalama na kuruhusu Watu kufanya shughuli zao hadi usiku.