Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 27Article 554047

Habari za Afya of Friday, 27 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Waziri Mkuu akereka kuzorota mradi wa Afya

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, hajaridhishwa na ujenzi wa Hospitali ya mkoa wa Katavi ambao ulianza tangu 2018 na hadi sasa umekamilika kwa asilimia 48 pekee na kumuagiza Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, kubaki mkoani humo ili kubadilisha mfumo wa ujenzi wa hospitali hiyo.

Ametoa kauli hiyo wakati alipotembelea Mradi huo wa maendeleo mapema hii leo, na kukuta mapunufu makubwa ya kiutendaji yaliyopelekea kuzorota kwa ujenzi wa hospitali hiyo.

Aidha, amewataka wakazi wanaoishi katika maeneo ya karibu na mradi huo kuimarisha ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za watu wanaoingia bila kufuata utaratibu katika mradi huo.