Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 24Article 559456

Habari za Mikoani of Friday, 24 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Waziri Mkuu amefika msibani kwa Mrema

Waziri Mkuu akitoa salamu za pole kwa kiongozi wa TLP Waziri Mkuu akitoa salamu za pole kwa kiongozi wa TLP

Waziri Mkuu, Kassim MAJALIWA amefika nyumbani kwa Mwenyekiti wa Chama cha (Tanzania Labor party) TLP Augustino Lyatonga eneo la Kiraracha Mkoani Kilimanjaro na kutoa pole kwa familia kufuatia kifo cha Mke wa Mzee Mrema, Bi. Rose Mrema aliyefariki Septemba 16, 2021 katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waombolezaji Waziri Mkuu amewapa pole ndugu, jamaa pamoja na familia ya Marrhemu na kuwataka kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu na kumuombea marehemu ili kuwapa faraja wanafamilia.

Waziri Mkuu amempa pole Mzee Mrema na kusema alikuwa ni kiongozi mchapakazi ma mtumishi mwema “Tunatambua mchango wako na hatuwezi sahau mchango wako Serikalini na ndio maana Rais Samia na Makamu wa Rais walituma salamu za pole, hii inaonesha mahusiano mazuri tuliyonayo”. Waziri Mkuu.