Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 26Article 553825

Habari za Mikoani of Thursday, 26 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Waziri Mkuu ametembelea ujenzi wa Bandari Katavi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu , Kassim Majaliwa ametembelea na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Bandari ya Karema katika wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, ambayo ujenzi wake umefikia asilimia hamsini.

Katika ziara hiyo ambayo Waziri Mkuu alifuatana na Watendaji wakuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi pamoja na Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA, Waziri Mkuu amewaambia wananchi kuwa ameridhishwa na kazi inayoendelea.

Aidha amesema serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia,imedhamiria kukamilisha miradi yote ya kimkakati pamoja na kuanzisha mingine lengo likiwa ni kuwawezesha wananchi kupata huduma muhimu na kuinua uchumi wa nchi.