Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 26Article 553783

Habari Kuu of Thursday, 26 August 2021

Chanzo: millardayo.com

Waziri Mkuu awajibu wanaopotosha kuhusu Chanjo ya Corona (Video+)

Waziri Mkuu awajibu wanaopotosha kuhusu Chanjo ya Corona (Video+) play videoWaziri Mkuu awajibu wanaopotosha kuhusu Chanjo ya Corona (Video+)

Akizungumzia kuhusu ugonjwa wa UVIKO 19, Waziri Mkuu amewataka wananchi wafuate maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya katika kujinga na ugonjwa huo na pale wanapoona dalili ambazo hawazielewi wawahi katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa uchunguzi na matibabu.

“Kama mnavyofahamu, kuwa dunia nzima ipo kwenye wimbi la tatu la UVIKO 19. Janga hili lipo nchini na limesababisha baadhi ya ndugu zetu kupoteza maisha na wengine kuendelea kuugua. Kwa msingi huo ni muhimu kwetu kuendelea kuchukua tahadhari kwa kujikinga na maambukizi ya UVIKO 19.”- Waziri Mkuu

Amesema kuwa chanjo ya UVIKO 19 inapatikana na inasambazwa nchini kote ikiwemo hapa Dodoma ambapo huduma hiyo inatolewa katika vituo 89 ndani ya mkoa.

“Sambamba na vituo hivi, pia ipo huduma ya mkoba (mobile) ambapo watumishi wa afya wanakwenda katika maeneo yenye watu wengi ikiwemo makampuni ya ujenzi na kutoa huduma”- Waziri Mkuu