Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 24Article 553336

Diasporian News of Tuesday, 24 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Waziri Mwigulu: "Muungano wa Tanzania unazidi kuimarika"

Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Mwigulu Nchemba amesema muungano wa Tanzania unazidi kuimarika baada ya kikao cha pamoja cha Mawaziri wa serikali zote mbili kukabaliana kuondosha kero kadhaa ikiwemo suala la fedha.

Waziri huyo amaeyasema hayo mara baada ya kikao cha Mawaziri na makatibu wakuu wote wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) cha kujadili kero zinazoukumba Muungano wa Tanzania.

Hata hivyo tangu kuanzishwa utaratibu wa kushughulikia hoja za Muungano kupitia vikao vya kamati ya pamoja ya SMT na SMZ mwaka 2006, hoja 25 zimejadiliwa na mpaka sasa hoja saba zimepatiwa ufumbuzi huku hoja 18 zikiendelea kutafutiwa ufumbuzi.