Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 11Article 584893

Habari Kuu of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Waziri Nape aguswa na vifo vya waandishi wa habari Mwanza "Nimepokea kwa Masikitiko"

Waziri Nape aguswa na vifo vya waandishi wa habari Mwanza Waziri Nape aguswa na vifo vya waandishi wa habari Mwanza

Gari la Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mwanza lililokuwa kwenye ziara ya RC wa Mwanza limepata ajali eneo la Busega likiwa linaelekea Ukerewe kupitia Bunda.Sasa Miongoni mwa viongozi walioguswa na ajali hiyo ni Waziri wa Habari Nape Nahuye ambae kupitia ukurasa wake wa twitter ameyaandika haya.“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali ya gari iliyosababisha vifo vya Maafisa Habari, Waandishi wa Habari wa Mwanza na Wananchi. Natoa pole kwa Familia za Marehemu, Waandishi wa Habari wote, ndugu, jamaa na marafiki. Mungu aziweke mahali pema roho za marehemu wote, Amina”- Waziri Nape Nnauye