Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 20Article 552676

Habari Kuu of Friday, 20 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Waziri Ummy apiga marufuku wakandarasi wa nje

Ummy Mwalimu, Waziri wa Tamisemi Ummy Mwalimu, Waziri wa Tamisemi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ummy Mwalimu amepiga marufuku kutumia wakandarasi wa nje ya halmshauri husika huku akisisitiza kuwa fedha hizo zirudi kwa Watanzania kwa kuhakikisha kazi hizo zinafanywa na mafundi wa eneo husika.

Ameyasema hayo wakati akithibitisha kupokea Fedha hizo zilizotoka na Tozo za miamala ya simu, Waziri huyo pia amewasisitiza wakandarasi kuwajibika ipasavyo ili kuzitendea haki fedha hizo zilizotoka na jasho halali la mtanzania huku akiwataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanawatumia wakandarasi wa ndani ili wanufaike na miradi inayofanyika katika maeneo yao.

Ujenzi wa vituo hivyo 90 vya afya unategewa kuanza mapema iwezekanavyo ikiwa ni awamu ya kwanza ya makusanyo ya tozo hizo.